Camavinga haondoki Real Madrid

0
154

Mabingwa wa Hispania, Real Madrid wameeleza kuwa hawana mpango wa kumwachia Eduardo Camavinga, kwani bado wanahitaji huduma yake.

Kwa mujibu wa mwandishi mashuhuri wa michezo duniani, Fabrizio Romano, pande zote mbili zimekanusha tetesi kuwa kiungo huyo raia wa Ufaransa atatolewa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Camavinga alisajiliwa na Real Madrid kwa dau la TZS bilioni 75 hadi mwaka 2027 akitokea Rennes, lakini amekuwa akipata ushindani mkubwa wa namba akichuana na Toni Kroos, Luka Modric na Federico Valverde.

Vinara wa Ligi Kuu ya England, Arsenal, walihusishwa kuitaka huduma ya kiungo huyo ikiwa ni mkakati wa kujiimarisha ili kutwaa taji hilo wanalolimendea baada ya takribani miaka 20.