Nukuu za Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

0
278

“Tuna kesi zenye ushahidi watanzania wanauza nyumba zao ili kugharamia matibabu ya mgonjwa, Bima ya Afya ni moja ya sehemu ya kumkomboa mwananchi maskini kwa sababu atapata huduma za matibabu bila ya kikwazo cha fedha.”

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

“Tumesema Bima ya Afya kwa wote ni lazima ila hakuna kosa la kisheria hapo, hakuna mtanzania atakamatwa, kuwekwa ndani au kufungwa kwa kukosa Bima ya Afya. Ila tunakwambia ukitaka kupata leseni ya biashara basi uwe na Bima ya Afya.”
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
“Tumekwenda Rwanda, Ghana hizi ni nchi za Afrika. Mfano Rwanda polisi anakusimamisha barabarani anakagua Bima ya Afya ipo wapi, sisi tunauliza bima ya gari tunakagua matairi ila wenzetu wanakagua bima ya afya kwa sababu ni lazima.”

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
“Asilimia 99 ya waliokata bima ya afya kwa hiyari, karibu wote wamekata bima ya afya wakiwa wagonjwa.”
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu