Wanawake watakiwa kupaza sauti kukemea ukatili wa kingono

0
200

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Gerson Msigwa, amewahimiza wanawake katika vyumba vya habari kupaza sauti zao kukemea ukatili wa kingono katika maeneo yao ya kazi.

Msigwa ameyasema hayo katika mkutano wa kwanza wa wahitimu wa mafunzo ya uongozi kwa wanawake wanahabari Tanzania (Women in News) ambao umefanyika leoJijini Dar es Salaam.

Msigwa amesema “Ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyumba vya habari upo, hata Mimi ni shahidi wa mke wangu amewahi kupitia nikishuhudia” amewaahidi Wahitimu hao wa tangu 2016 hadi sasa kuendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili waandishi wa habari wanawake:.

Msigwa ameongeza kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo mstari wa mbele kupigania haki zao hivyo nao wanachokipata katika mafunzo hayo yawajenge na kujiamini kuendelea kufanya makubwa zaidi kwa maendeleo ya Tanzania.

Mkutano huo mkubwa ni wa kwanza kufanyika tangu kuanza kwa mafunzo ya wanawake katika vyumba vya habari 2016 hadi 2022 ulio chini ya uratibu wa shirika la kimataifa la WAN IFRA, unalenga kuongeza ujasiri kwa waandishi wanawake na sauti katika vyumba vya habari huku wakifanya kazi kwa uhuru pamoja na wanaume bila kufanyiwa ukatili wa kingono.