Ronaldo, Messi uso kwa uso leo

0
285

Nahodha wa timu ya soka ya Ureno Christiano Ronaldo, leo atawaongoza nyota wanaoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia dhidi ya PSG ya Lionel Messi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa matajiri wa Saudi Arabia wanapigana vikumbo kununua tiketi kwa bei ya juu ambapo imeelezwa kuwa kila mmoja anataka kununua tiketi kwenye maeneo yenye hadhi ya VVIP.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo na Messi kukutana tangu walipokutana wakati wa mchezo baina ya Barcelona na Juventus katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya msimu wa 2020/2021.