Mafunzo ya SDF yawanufaisha vijana

0
187

Vijana 600 wamenufaika na mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi (SDF) yanayotolewa kwa vijana wa Unguja na Pemba kupitia mpango wa ufadhili kwa Vijana kutoka kaya maskini na wanaoishi katika mazingira magumu unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

TEA imepewa jukumu la kusimamia na kutekeleza mpango huo na wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kuwafikia vijana kutoka makundi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu walio katika kaya zilizosajiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).