Mradi wa umeme JNHPP wafikia 80.2%

0
111

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato amesema utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115 za umeme umefikia asilimia 80.2.

Naibu Waziri Byabato ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wizara ya Nishati ikitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini .

“Kwa sasa utekelezaji wa mradi unaenda kwa kasi ambapo hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2022 umefikia asilimia 80.22, aidha mnamo tarehe 22 Desemba 2022 zoezi la kuanza kujaza maji katika bwawa la JNHPP lilifanyika kwa kufunga mageti ya njia ya mchepusho.” amesema Byabato

Kuhusu kazi ya ujazaji maji katika bwawa lhilo Byabato amesema, hadi kufikia tarehe 16 mwezi huu kimo cha maji cha bwawa kilifikia mita 112.48 kutoka usawa wa bahari kutoka mita 74 Desemba 22 mwaka 2022.