Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewataka Majaji nchini kuzingatia weledi, kufuata misingi ya kisheria na kutenda haki katika kazi zao.
Dkt. Tulia ameyasema hayo mkoani Tanga wakati akifungua mkutano wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
“Ni wakati wa kusimama imara kuweza kutimiza majukumu yenu hata pale kwenye vikwazo na changamoto za kijamii, kiimani na kitamaduni”. amesisitiza Dkt. Tulia
Ameongeza kuwa Bunge lipo tayari kupokea maoni ya mabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati, ili kuzifanyia maboresho kwa lengo la kuhakikisha haki za makundi mbalimbali katika jamii zinalindwa.