Makambo Aondoka Yanga

0
196

Yanga SC imeachana na mshambuliaji wake kutoka DR Congo, Heritier Makambo ambaye alirejea Yanga Agosti 2021 akitokea Horoya AC ya nchini Guinea alikodumu kwa misimu miwili tangu mwaka 2019.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, Yanga imeandika “𝗔𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 Heritier Ebenezer Makambo. Tunakutakia kila la heri na mafanikio.”

Makambo anakuwa mchezaji wa pili kuondoka katika dirisha dogo la usajili baada ya klabu hiyo kuachana na Yacouba Songne.