DART watangaza nauli mpya za ‘Mwendokasi’

0
170

Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), umetangaza nauli mpya zitakazoanza kutumia Januari 16, 2023 na kuweka bei za nauli hizo katika ruti tofauti.

Taarifa hiyo imeonesha kuwa nauli katika njia kuu ya Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani na Kimara-Morocco itakuwa Sh750.

Kimara-Mbezi nauli itakuwa Sh500 wakati ile ya Kimara- Kibaha na Kimara-Mlongazila itakuwa Sh 700, Gerezani – Muhimbili itakuwa Sh750.