Fedha za wawekezaji zipo salama

0
148

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza pesa zao katika mfuko unaoaminika wa ‘Faida Fund’ uliopo chini ya Watumishi Housing Investment.

Ameyasema hayo akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ufunguzi rasmi wa mfuko huo utakaowawezesha Watanzania wa kipato cha kati na chini kuwekeza katika vipande na masoko ya Fedha na Mitaji bila makato.

“Kupitia Faida fund… fedha za wawekezaji zipo salama,” amesisitiza Waziri Mhagama.

Aidha, amewapongeza Watumishi Housing kwa kuongeza wigo wao wa kufanya kazi kutoka kwenye uwekezaji wa nyumba hadi kwenye mfuko wa kununua vipande.

Wanaoweza kujiunga na mfuko huu ni Watanzania wote wenye huduma za kuendana na imepanua wigo wake na hivyo kutoa huduma zake kwa watumishi wa serikali na wananchi wa kawaida.