TMA yatahadharisha mvua kubwa mikoa 6

0
239

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa huku ikitoa angalizo la mvua kubwa kunyesha leo Jumamosi katika maeneo machache ya mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Singida na Dodoma.

Katika taarifa hiyo, TMA imeeleza athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni baadhi ya makazi kusombwa na maji, maeneo ya mabondeni kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji.