Uteuzi watendaji wakuu wa baraza la wafanyakazi TBC

0
114

Baraza la Wafanyakazi la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limewateua na kuwapitisha kisheria watendaji wakuu wa baraza hilo, Malembo Simbano kwa ngazi ya Katibu na Anna Malimbo kama Katibu Msaidizi ambao watahudumu katika baraza jipya linalotarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Awali watendaji hao walikuwa wakitumikia nafasi hizo kwa kipindi kilichopita ambapo sasa wamechaguliwa kuendelea na uongozi kwa kipindi kingine.