BOT yatoa elimu ya utunzaji wa fedha

0
577

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imewataka Watanzania wote kuzingatia  njia salama za utunzaji wa fedha hasa noti ili kuwezesha fedha hizo kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu na hivyo kupunguza gharama za uchapishaji wa noti mpya mara kwa mara.

Wito huo umetolewa na Meneja Msaidizi wa Kitengo cha Uhusiano cha BOT, – Vicktoria Msina  wakati wa semina iliyohusu utunzaji wa fedha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa Wakazi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.