Rais wa heshima wa Simba ateta na Wachezaji

0
152

Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji (Mo Dewji) amekutana na wachezaji wa timu hiyo na kuzungumza nao ambao katika kambi mjini Dubai.

Katika mazungumzo hayo Mo amewashukuru wadhamini, mwenyekiti na wajumbe wa bodi wanaomaliza muda wao, pia amewatakia wanachama mkutano mkuu mwema.

Pia, amewashukuru mashabiki na mtendaji mkuu anayemaliza muda wake, Barbara Gonzalez na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa timu hiyo kufika malengo waliyojiwekea mwaka huu ikiwemo kufika nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Klabu ya Simba ipo jijini Dubai kwa kambi ya siku saba kwa mwaliko rasmi wa Rais huyo ambapo pia watapata fursa ya kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Al Dhafra FC na CSKA Moscow ya Urusi.