Uzinduzi wa kituo cha TBC Inyonga, Mlele

0
334

Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kurusha matangazo ya redio TBC Taifa na TBC FM kilichopo Inyonga, Mlele mkoani Katavi.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye @napennauye anatarajiwa kuzindua kituo hicho muda mfupi ujao leo Januari 10, 2023.

Kituo hicho kimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) @ucsaftz

Matangazo yatakujia mbashara kupitia TBC1, TBC2, TBC Taifa, TBC FM na mtandao wa YouTube wa TBC online.