Pauni Milioni 300 kuisuka upya Real Madrid

0
488

Rais wa klabu ya Real Madrid, -Florentino Perez amemuahidi kocha mpya wa kikosi hicho Zinedine Zidane kitita cha Pauni Milioni Mia Tatu kwa ajili ya matumizi ya usajili wa wachezaji watakaosuka upya kikosi hicho.

Jumatatu Aprili 11 mwaka huu Real Madrid ilimtangaza Zinedine Zidane kuwa kocha mpya wa timu hiyo,  ikiwa imepita miezi Kumi tangu aachane na kibarua cha kukinoa kikosi hicho ambacho alikipa mafanikio makubwa katika kipindi cha muda mfupi.

Zidane anarejea tena Santiago Bernabeu kurithi mikoba ya Santiago Solari aliyetimuliwa kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ya miamba hiyo ya soka Barani Ulaya, hasa baada ya kufungashiwa virago na Ajax Amstaderm kwenye ligi ya mabingwa Barani Ulaya pamoja na kutupwa nje ya mbio za kuwania ubingwa wa La Liga.

Perez amedhamiri kuirejesha Galacticos kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014 na amepania kunasa saini ya nyota Watatu ambao ni Neymar kutoka PSG, Eden Hazard kutoka Chelsea, Christian Eriksen kutoka Tottenham Hotspur na ikiwezekana hata Kylian Mbappe kutoka kwa matajiri wa Ufaransa, -PSG.

Katika mpango huo wa matumizi ya Pauni Milioni Mia Tatu, Real Madrid pia itauza baadhi ya nyota wake ambao wanaonekana kushuka viwango wakiweo Gareth Bale na kiungo wa kimataifa wa Croatia,- Luca Modric.