Bale atundika daluga

0
203

Mchezaji wa kimataifa kutoka Wales, Gareth Bale ametangaza kustaafu soka la kimataifa na klabu.

Kupitia taarifa rasmi aliyoichapisha, Bale amesema amekuwa na wakati mzuri kwa misimu 17 ya kucheza soka la ushindani.

Amewashukuru wote waliomuunga mkono na kumpa ujasiri wa kucheza mchezo huo anaoupenda tangu akiwa na miaka 9 wakiwemo wazazi wake, makocha, wachezaji wenzake pamoja na mkewe na watoto ambao walikuwa nae kwa kipindi chote cha kusakata kabumbu.

Bale amewahi kucheza Southampton, Tottenham, Real Madrid na LAFC ya nchini Marekani.