Maandalizi uzinduzi kituo cha TBC – Inyonga, Mlele

0
286

Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Fiberto Sanga amekagua maandalizi ya uzinduzi wa kituo cha kurusha matangazo ya Redio TBC Taifa na TBC FM kilichopo Inyonga, Mlele mkoani Katavi ambapo alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Steven Kagaigai aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi.

Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Katavi, Mhandisi Isack Kamwelwe naye ametembelea kituo hicho.

Kituo hicho kitazinduliwa Januari 10, 2023 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.