Ronaldo kuibeba Juve leo?

0
475

Kivumbi cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kinaendela usiku wa leo Aprili 12 ambapo michezo miwili inachezwa kutafuta timu mbili zitakazotinga hatua ya robo fainali.

Baada ya mchezo wa kwanza kunyukwa mabao Mawili kwa Bila, Kibibi kizee cha Turin,-Juventus wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kupindua matokeo mbele ya wabishi Atletico Madrid wanaosafiri hadi mjini Turin kutafuta walau sare tu kupenya robo fainali.

Juventus watakuwa wakitegemea zaidi huduma ya mshambuliaji wake Christiano Ronaldo mwenye uzoefu mkubwa na michuano hiyo kupindua matokeo mbele ya vijana wa Diego Simione wanaosifika kwa kuwa na ukuta mgumu ukiongozwa na mkongwe Diego Godin.

Mchezo mwingine unaochezwa siku ya leo, matajiri Manchester City wakiwa na faida ya ushindi wa mbao Matatu kwa Mawili walioupata ugenini,  watakuwa nyumbani kwenye dimba la Etihad kumenyana na Schalke 04 ya Ujerumani, mchezo  ambao kocha wa Man City,- Pep Guardiola anasema atatoa nafasi kwa wachezaji chipukizi kuonesha uwezo wao.

Kesho Jumanne Aprili 13,  hatua ya 16 bora itahitimishwa kwa michezo miwili ambapo FC Barcelona watakuwa nyumbani Camp Nou kumenyana na Olmpic Lyon ya Ufaransa huku majogoo wa jiji Liverpool wakisafiri kuwafuata The Bavarians, Bayern Munchen pale Allianz Arena mjini Munich.