Uteuzi wa Gavana BoT

0
202

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Emmanuel Tutuba kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuchukua nafasi ya Profesa Florence Luoga ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya uteuzi huo Tutuba alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Aidha, Rais Samia pia amemteua Dkt. Natu El Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua nafasi ya Emmanuel Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania.

Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO).

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Emmanuel Tutuba kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuchukua nafasi ya Profesa Florence Luoga ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya uteuzi huo Tutuba alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Aidha, Rais Samia pia amemteua Dkt. Natu El Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua nafasi ya Emmanuel Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania.

Dkt. Mwamba alikua mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam na mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KADCO)