Man City yaichapa Chelsea

0
192

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Chelsea usiku wa Alhamisi katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Bao pekee la Manchester City lilifungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jack Grealish.

Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha alama 39, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 17.

Kwa upande wao Chelsea baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na alama zao 25 za mechi 17 nafasi ya 10.