Kocha wa Simba SC amesema baada kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea Zanzibar, visiwa hivyo havikaliki tena.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa Simba na KVZ amesema hawana la kufanya visiwani humo, hivyo wanarudi Dar es Salaam kujiandaa na mashindano ya kimataifa.
Mchezo wa kwanza Simba ilifungwa goli moja na Mlandege na leo imeshinda goli moja kwa kuifunga KVZ.