Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Kampala nchini Uganda kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania na kulakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Philemon Mateke katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe.
Makamu wa Rais amekwenda nchini Uganda kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa Africa Now Summit 2019 utakaofanyika kuanzia Jumanne Machi 12.
Katika uwanja huo wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe, Makamu wa Rais pia amelakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima