Kiboksi cha taarifa za mwenendo wa ndege chapatikana

0
335

Kifaa maalum cha kurekodi taarifa za mwenendo wa ndege maarufu kama black box cha ndege ya Shirika la Ethiopia iliyoanguka Jumapili Machi 10 mwaka huu muda mfupi baada ya kuruka kimepatikana.

Kifaa hicho cha kurekodi sauti na taarifa za kidigitali za ndege hiyo kimepatikana katika eneo ulipoangukia mkia wa ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX 8.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa, -Ethiopia kwenda Nairobi nchini Kenya ambapo ilianguka ndani ya dakika sita baada ya kupaa na kuua watu wote 157 waliokuwamo ndani.