Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es salaam wakimsubiria Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atafanya mazungumzo na viongozi hao.
Mkutano huo ni sehemu ya Maridhiano ya kisiasa ambayo yanaendelea kusimamiwa na serikali pamoja na vyama vya siasa hapa nchini.