Kiongozi Mstaafu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict XVI (95) amefariki dunia katika makazi yake Vatican.
Katika taarifa yake Vatican imesema “Kwa masikitiko ninawajulisha kuwa Papa Mstaafu, Benedict XVI amefariki dunia leo saa 9:34 katika Monasteri ya Mater Ecclesiae huko Vatican.”
Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda usiozidi miaka minane, kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII alipojiuzulu mwaka 1415.
Siku ya Jumatano, Papa Francis alitoa wito kwa hadhira yake ya mwisho ya mwaka huko Vatican kusali sala maalum kwa ajili ya Papa Benedict ambaye alisema alikuwa mgonjwa sana.
Papa Benedict ambaye jina lake kamili ni Joseph Ratzinger ni mzaliwa wa Ujerumani.