Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia michezo mitatu mchezaji wa Yanga, Abdallah Shaibu maarufu kama Ninja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union ya mkoani Tanga.
Afisa Habari wa TFF, – Clifford Ndimbo amesema kuwa shirikisho hilo limejiridhisha kuwa Shaibu alitenda kosa hilo kwenye mchezo kati ya Coastal na Yanga baada ya yeye mwenyewe kukiri.
Ndimbo amesema kuwa mchezaji huyo ana haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.