Bandari ya Tanga kurejesha hadhi ya mkoa huo

0
129

Bandari ya Tanga inatarajiwa kurejesha hadhi ya mkoa huo ambao miaka ya nyuma ulikuwa unashika nafasi ya pili kwa uchumi imara Tanzania, ukitanguliwa na Dar es Salaam.

Hayo yamesmemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga, Masoud Mrisha wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika bandari hiyo ili kujionea jitihada za Serikali katika kubresha bandari hiyo ya kimkakati.

Masoud amesema Katika awamu ya kwanza ya uboreshaji wa bandari hiyo Serikali ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 172 kwa lengo la kuongeza kina kutoka mita 3 hadi mita 13 ili kuweza kuingiza meli hadi sehemu ya kushushia mizigo.

Aidha, katika awamu ya pili serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 256 kwa ajili ya kuboresha magati 2 yenye urefu wa mita 450, kuongeza mita 50 upande wa Mashariki na mita 92 Magharibi.

Bandari ya kimkakati ya Tanga itakapokamilika inatarajiwa kuwa na uwezo wa kihudumia shehena ya kutoka tani laki 750,000 mpaka tani milioni 3,000,000 pamoja na kufungua fursa za kiuchumi na pato la Taifa.

Serikali imeendelea na juhudi za kuboresha Miundombinu ya usafirisha ikiwepo Bandari za hapa nchini ili kuleta ufanisi katika kukuza pato la Taifa na Ajira nyingi kwa Watanzania.