Mtangazaji mashuhuri wa kituo cha televisheni cha KBC nchini Kenya, Catherine Kasavuli amefariki dunia huku akitaja mambo 6 muhimu ya kuzingatia wakati wote wa maisha yako.
Kasavuli ambaye alikuwa akiongoza kipindi maarufu cha habari ‘Legends Edition’ katika kituo hicho amefariki dunia kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimkabili kwa kipindi kirefu.
Kasavuli ameitaja familia yake kama ndio kila kitu na kuwataka wafuasi wake kujenga amani na kuwa mwema kwao hata kama unahisi tofauti.
- Kila siku tegemea nguvu ya Mungu, sali kwa kadiri uwezavyo na hasa ukiwa na nguvu za kutosha.
- Kama una marafiki au watu wako wa karibu walau wawili kila siku washukuru kwa kuwa ni watu muhimu.
- Usipoteze matumaini, endelea kuamini na kujipa moyo.
- Upende mwili wako na uheshimu.
- Mwisho, kila siku kuwa mwema, itakusaidia baadaye.
Akamalizia kwa kusema, Asante watu wazuri nawapenda wote
Akaweka na hashtag