Kwa mara ya kwanza Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambaye amewahi kuwa mlimbwende wa Temeke na mshindi wa pili wa shindano la urembo Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo amemtambulisha mtoto wake hadharani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo ameandika “Her name is Totoo” [Jina lake ni Totoo] “Call me mama Totoo” [Niite Mama Totoo], akamalizia kwa kuandika “Glory to God,” [Utukufu kwa Mungu].
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuchapisha picha akiwa na mtoto wake wa kike tangia alipojifungua hivi karibuni.