Wabunge, Madiwani wapiga magoti kumshukuru Rais

0
144

Baadhi ya wabunge na madiwani wa mkoa wa Njombe wamepiga magoti kumshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameguswa na matatizo ya barabara za mkoa huo na kutoa fedha za kuzijenga.

Hatua hiyo imeongozwa na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga maarufu Jah People ambaye aliwaita mbele madiwani waliohudhuria hafla ya utiaji saini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara katika wilaya ya Makete mkoani Njombe na kisha kuwaamuru kupiga magoti na kushukuru kwa namna wanavyopendelewa na Rais.

“Nimewaita hapa mbele ili kwa pamoja tumshukuru Rais wetu kwa namna alivyotumiminia mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za wilayani Makte,” amesema Sanga

Barabara zitakazokabidhiwa kwa wakandarasi hii leo ni pamoja na ile ya kutoka Isyonje – Kikondo yenye urefu wa kilomita 92.6 na Kitulo – Iniho yenye urefu wa kilomita 36.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha zege.