Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini hii leo kuelekea Kampala nchini Uganda kushiriki kwenye mkutano wa mwaka wa Africa Now Summit.
Katika mkutano huo wa siku Mbili, Makamu wa Rais anamwakilisha Rais John Magufuli.
Mkutano huo utafunguliwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huo, mkutano utakaokuwa na mada mbalimbali ikiwemo ile ya uongozi itakayowasilishwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wengine watakaowasilisha mada wakati wa mkutano huo ni Rais Abdel Fattah El Sisi wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Makamu wa Rais wa Kenya, – William Ruto na Waziri Mkuu wa Ethiopia, – Ahmed Abiy.