Maelekezo ya Rais Samia kwa Waziri Mbarawa

0
126

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameyataja maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Ibanda – Kajunjumele – Kiwira Port,  Kajunjumele- Itungi Port alipokuwa akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mbeya katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara hizo.

Amesema Rais Samia ameelekeza utiaji saini wa mikataba hiyo ufanyike kwa kushuhudiwa na wananchi na si ofisini kama ilivyokuwa ikifanyika kwa miradi ya namna hiyo nyakati  za nyuma.

Vilevile amesema Rais Samia ameelezeka kufanyika upya mapitio ya tathimini ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa kuwa tathimini ya awali iliyofanyika mwaka 2018 imeonekana kupitwa na wakati.

Ameongeza kuwa Rais ameelekeza mradi huo kujengwa kwa teknolojia ya kisasa pamoja na kupatikana kwa mkandarasi mwenye viwango atakayeweza kuijenga barabara kwa teknolojia ya kisasa.

Prof. Mbaraba ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutunza miundombinu ya barabara hizo kusudi idumu muda mrefu,  pia wampe mkandarasi ushirikano kusudi aweze kutekeleza majukumu yake kama ipasavyo.