MRADI UTAIUNGANISHA TANZANIA NA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA

0
142

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila amesema moja ya manufaa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ibanda- Kajunjumele – Kiwira Port,  Kajunjumele- Itungi Port yenye kilomita 32 ni kuiunganisha Tanzania na nchi za Kusini mwa Afrika kupitia kiungo cha barabara kuu ya Mbeya.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani Mbeya itakayojengwa na mkandarasi kutoka Uturuki, amesema mradi huo hadi kukamilika utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 38.359  bila kujumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo imesamehewa na Serikali.

Mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya mienzi 24, na baada ya kukamilika kwa mradi huu utakuwa katika kipindi cha matazamio kwa muda wa mienzi 12.