Martinez achora tattoo ya Kombe la Dunia

0
146

Kipa wa timu ya Taifa ya Argentina, Emiliano Martinez amechora tattoo ya Kombe la Dunia ambalo wamelinyakua mwaka huu katika michuano iliyofanyika Qatar.

Martinez anakuwa mchezaji wa pili kutoka katika timu hiyo kujichora tattoo akitanguliwa na mwenzake Angel Di Maria.

Kipa hiyo anayekipiga katika klabu ya Aston Villa ya Uingereza amechora kombe hilo kwenye mguu wake wa kushoto, eneo ambalo mpira ulimgonga na kuokoa hatari kwenye goli la Argentina katika dakika za mwisho za mchezo. Endapo, asingeokoa shuti hilo, pengine Argentina wasingetwaa taji hilo kubwa zaidi duniani.