Ujumbe kutoka serikali ya Ethiopia uko njiani kuelekea eneo la Kaskazini la Tigray kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani ya mwezi uliopita.
Huu ni ujumbe wa kwanza wa ngazi ya juu wa shirikisho ambao umesafiri hadi Tigray katika miaka miwili, Serikali imesema Spika wa Baraza la Wawakilishi Tagesse Chafo ndiye anayeongoza ujumbe huo.
Serikali ya shirikisho na vikosi vya Tigray vilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano kabisa mnamo Novemba 2, baada ya miaka miwili ya mapigano ambayo yalisababisha vifo vya maelfu na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.
Mkataba wa ufuatiliaji wa kuwapokonya silaha wapiganaji wa kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF), dhamana ya kupata misaada ya kibinadamu na kuingia kwa wanajeshi wa Ethiopia katika mji mkuu wa Tigray wa Mekele ulitiwa saini Novemba 12.
Chanzo BBC Swahili
