Mongella: Tuiombe nchi yetu, tuipende nchi yetu

0
158

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema sambamba na kufuata neno la Mungu kwa matendo amewakumbusha Watanzania katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi  wakumbuke pia kuombea nchi ya Tanzania katika  nyanja tofauti.

John Mongella ameyasema hayo katika Ibada ya Krismasi Kitaifa inayofanyika katika Kanisa Presbyterian jijini Arusha.

Pia, ameyapongeza makanisa kwa umoja wao na kazi ya makanisa katika jamii.
“Kanisa linafanya mambo mengi sana kwa wananchi.”

Mongella amemaliza kwa kuwatakia wakazi wa Arusha pamoja na Watanzania wote heri ya Krismasi na mwaka mpya