Bwawa la Julius Nyerere kuanza kujazwa maji leo

Mradi wa Kufua Umeme

0
207

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atafunga njia ya mchepusho ya maji na tayari kuanza ujazaji maji kwenye Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lililopo mkoani Pwani.

Mradi huo wa kihistoria nchini Tanzania utazalisha umeme megawatts 2115 na kugharibu shilingi trilioni 6.55.

Hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu, Mradi wa (JNHPP) umefikia asilimia 78.68 huku ukiendelea kushika kasi ya ujenzi katika hatua iliyobakia.

Handaki la kuchepusha maji hayo lina urefu wa mita 700, sawa na urefu wa viwanja saba vya mpira wa miguu; lilijengwa miaka mitatu iliyopita na kugharimu shilingi bilioni 235.

Bwawa la Julius Nyerere litakalotumika kuzalisha umeme wa Megawatts 2115 lina jumla ya kilometa za mraba 916, na kulifanya bwawa hilo kuwa bwawa kubwa kuwahi kutengenezwa nchini Tanzania.