Ujenzi wa vyuo 62 vya VETA kuanza Januari

0
145

Serikali imeitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kukamilisha haraka michakato ya ndani na kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi katika wilaya 62 kuanzia Januari 2023.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa VETA kutekeleza agizo hilo akibainisha kuwa katika bajeti ya mwaka 2022/2023 serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo.

“Muanze ujenzi kwa mipango madhubuti ili watu waliopo nje wakiangalia waone kweli hii ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na taasisi zake zinafanya kazi inayotakiwa,” amekaririwa Waziri Mkenda

Katika hatua nyingine amesema kuwa uongozi wa VETA kwa asilimia kubwa una makaimu watendaji wengi hivyo mafanikio ya kazi hiyo pekee yatatoa fursa ya viongozi hao kupewa nafasi kubwa zaidi kwa kushikilia nafasi hizo na sio kukaimu.

Waziri Mkenda amesema kuwa VETA inafundisha elimu ya ufundi hivyo kupewa jukumu la ujenzi ni kutaka ionyeshe kwa vitendo ni kwa kiasi gani inafundisha taaluma inayoiweza.