Kosa la ujanani lahukumiwa uzeeni

0
151

Mahakama ya Kaskazini mwa Ujerumani imemtia hatiani mwanamke mwenye umri wa miaka 97 kwa kosa la kuua watu zaidi ya 10,000 wakati wa mauaji ya Holocaust, tukio lililotendeka akiwa kijana katika miaka ya 1940.

Kati ya mwaka 1943 hadi 1945, Irmgard Furchner alikuwa akifanya kazi kama katibu kazi ya mpigachapa kwenye kambi ya mateso ya Stutthof.

Furcher amepatikana na hatia ya kuwa msaidizi wa mauaji ya kimfumo ya maelfu ya watu akitumikia nafasi ya ukatibu.

Kesi ya Furcher iliendeshwa katika mahakama ya watoto, kwa kuwa  Furchner alikuwa kijana wakati uhalifu huo ukitendeka.

Hata hivyo wakati wa kusomewa mashtaka mwanamke huyo wa miaka 97 aliomba msamaha kwa kile kilichotokea na kusema kuwa anajuta kuwa moja wa watu waliokuwa kwenye kambi hiyo ya mateso.

Takriban watu 65,000 wanadhaniwa kufa katika mazingira ya kutisha katika kambi hiyo, wakiwemo wafungwa wa Kiyahudi, Wapoland wasio wayahudi na wanajeshi wa Soviet.