Radi yaua mwanafunzi

0
161

Mwanafunzi mmoja wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki dunia baada ya kupigwa na radi.

Calister Haule (15) mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Lugalo, Iringa alipatwa na ajali hiyo wakati akifungua mbuzi chini ya mti wa mkorosho wakati hali ya hewa ikiwa ni ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Mbali na kifo hicho, nyumba takribani 16 zimeezuliwa, na sita kubomoka. Mbuzi aliyekuwa akifunguliwa pia alikufa.