Ashitakiwa kwa kumtukana mwanae mitandaoni

0
240

Mwanamke mmoja huko Michigan anakabiliwa na mashitaka ya kutuma meseji zenye kusambaza chuki na uonevu kwa wanafunzi wadogo kwenye mitandao ya kijamii akiwemo mwanae wa kumzaa kwa namba ngeni.

Kendra Licari (42) anakabiliwa na mashitaka matano, ikiwa ni pamoja na kuvizia mtoto mdogo na kuzuia haki kutendeka, kulingana na malalamiko yaliyowasilishwa dhidi ya mama huyo.

Baada ya uchunguzi wa mwaka mzima kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na Shule ya umma ya Beal kufuatia bintiye na mpenzi wake kuripoti kupokea jumbe za kuwatishia.

“Hata tulipogundua kuwa haikuwa mtoto, hatukutarajia kwamba angekuwa mzazi,” William Chilman, msimamizi wa shule amekiambia chombo kimoja cha habari Marekani.

“Walipotufahamisha baadaye kwamba walikuwa wakishuku kuwa labda ni Licari, ilikuwa msihtuko kwetu sote, nadhani kila mtu aliyehusika,” Chilman aliongeza.

Anadaiwa kuficha kuonesha eneo lake na kubadili namba kila mara, na kuwasingizia wanafunzi wenzake na mwanae.

Licari, aliajiriwa na shule hiyo kama mkufunzi wa mpira wa kikapu na sababu za kufanya hivyo hazijajulikana.