Ranieri kwenda AS Roma?

0
627

Kocha wa zamani Chelsea, Leicester na Fulham, – Claudio Ranieri yupo kwenye nafasi nzuri ya kuteuliwa kuwa kocha wa mpito wa klabu ya AS Roma iliyomtimua kocha Eusebio Di Francesco.

Roma imemtimua Di Francesco siku moja tu baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa kufungwa mabao matatu kwa moja na FC Porto na kuondoshwa kwa jumla ya mabao Manne kwa Matatu kwenye hatua ya mtoano.

Roma imekua na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye siku za hivi karibuni ambapo kabla ya kufungwa na FC Porto ilikumbana na kichapo cha mabao Matatu kwa Nunge mbele ya Lazio kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Italia.

Claudio Ranieri aliyefukuzwa kazi na Fulham siku za hivi karibuni, amewahi kukinoa kikosi hicho cha AS Roma na anapigiwa chapuo ya kurudi tena Staidio Olimpico kuchukua mikoba ya Di Francesco aliyerithi mikoba kwa Luciano Spalleti ambaye alitimkia Inter Milan mwanzoni mwa msimu huu.