TAMISEMI , TET wateta

0
105

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI- Elimu, Dkt.Charles Msonde ameipongeza TET kwa kuweka maudhui ya elimu ya awali, MsingI, Sekondari na Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini katika mifumo wa kieletroniki, pamoja na kuweka vitabu vyote vya kiada katika Maktaba Mtandao.

Aidha, ameeleza kuwa ameguswa na kufurahishwa sana kwa TET kuweka vitabu vyote katika mfumo wa e-book jambo ambalo limerahisisha upatikanaji wa machapisho hayo na hivyo kurahisisha tendo al ufundishaji na ujifunzaji.

Pia alipata nafasi ya kutembelea studio za sauti na picha za TET pamoja na ghala la vitabu vya kiada vya kuanzia elimu ya Awali,Msingi na Sekondari lililopo EPZA ambako alielezwa namna kazi ya usambazaji na usafirishaji wa vitabu inavyofanyika.

Katika hatua nyingine, Dkt. Msonde ameahidi ushirikiano kwa TET katika masuala yote hususani kwenye suala la mafunzo kazini kwa walimu na kwenye matumizi ya Maktaba Mtandao ambapo atawahamasisha viongozi na walimu wote katika Halmashauri kushiriki katika mafunzo na kutumia Maktaba Mtandao hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET-Dkt. Aneth Komba amemshukuru Naibu Katiku Mkuu huyo kwa kutenga muda wa kuitembelea TET na kusema kuwa wataendelea kutekeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za kuboresha elimu kwa kuhakikisha kuwa majukumu yote ya TET yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.