UVIKO19 yarejea, shule zafungwa China

0
117

Ofisi ya Elimu ya Shanghai, China imeagiza madarasa kufanyika kwa njia mtandaoni kuanzia Jumatatu kutokana na kuongezeka kwa maambukizo ya UVIKO19 nchini humo.

Maambukizi ya UVIKO19 yamezidi kuongezeka tangu China ilipoondoa vizuizi wiki iliyopita, na kuna hofu kwamba ugonjwa huo unaweza kuenea kwa kasi katika idadi ya watu bilioni 1.4 wakati wa likizo za Krismasi na mwaka mpya.

Idadi ya maambukizo mapya 2,286 imeripotiwa siku ya Ijumaa, ikilinganishwa na 2,157 siku ya Alhamisi, Tume ya Kitaifa ya Afya China imesema.