Waandishi TBC watunukiwa tuzo

0
108

Waandishi wa habari wanne wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ni miongozi mwa waandishi wa habari waliotunukiwa tuzo na wizara mbalimbali kutokana na mchango wao katika kuandika habari za kijamii ambazo pia zinazihusu wizara hizo.

Waandishi hao ni Mwamini Andrew na Safina Yasini waliopokea tuzo kutoka wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Asher Thomas amepokea tuzo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi huku Rehema Sebabili akipokea tuzo kutoka wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.