Mazishi ya Kapembe

0
84

Mke na watoto wa Joachim Kapembe, mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) aliyefariki dunia tarehe 13 mwezi huu mkoani Kilimanjaro, wakiaga mwili wa mpendwa wao huko mkoani Tanga.

Mazishi ya Kapembe aliyefariki dunia baada ya kupata ajali ya baiskeli akishuka kutoka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro yanafanyika hii leo katika makaburi ya Kange mkoani Tanga.