Rais John Magufuli amesema kuwa serikali inathamini na itaendelea kuthamini kazi kubwa zinayofanywa na Wanawake nchini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.
Akizungumza na wanawake mbalimbali waliokuwepo uwanjani hapo, Rais Magufuli amewataka Wanawake nchini kuendelea kuhamasisha Umoja na Mshikamano wa Taifa.
Amesema kwa upande wa serikali, itahakikisha inawapatia Wanawake nchini fursa mbalimbali ili waweze kujiendeleza.
Rais Magufuli pia amewatakia heri Wanawake wote nchini katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yanye kauli mbiu inayosema kuwa “Badili Fikra kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”.