Rais Paul Kagame wa Rwanda ameondoka nchini hii leo baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku Mbili.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa ya Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Rais Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameagwa na mwenyeji wake Rais John Magufuli na viongozi wengine mbalimbali.
Akiwa hapa nchini, Rais Kagame amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli, mazungumzo yaliyohusu masuala ya kiuchumi kati ya Tanzania na Rwanda pamoja na Ukanda wa Afrika Mashariki.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kagame kufanya ziara hapa nchini akiwa kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.