Kenya yasherehekea miaka 59 ya Uhuru

0
441

Rais William Ruto wa Kenya, leo anawaongoza raia wa nchi hiyo kusherehekea miaka 59 ya Uhuru (Jamhuri Day), sherehe zinazofanyika katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Sherehe hizo zimeanza mapema leo asubuhi, na zinafanyika huku Taifa hilo likitajwa kuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukuaji wa sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia.

Rais Ruto anaongoza sherehe za Uhuru kwa mara ya kwanza tangu awe na wadhifa wa Urais.

Kenya ilipata Uhuru wake Desemba 12 mwaka 1963 kutoka kwa Uingereza.